Posted on 1 Comment

Uchanganuzi wa Sentensi Changamano

picha ya kishazi tegemezi

Kielelezo cha Kistari

Hii ni mbinu ya kimsingi ya kuchanganua sentensi. Mwanafunzi akielewa mbinu hii vizuri atakuwa na msingi mzuri wa kuchanganua sentensi yoyote kwa kutumia mishale,matawi na jedwali.

Sentensi changamano ni sentensi ambayo ina kishazi huru na kishazi tegemezi.

Mtahiniwa lazima aweze kutambua mambo haya ili aweze  kutenganisha kundi tenzi na kundi nomino.

Leo nitachanganua sentensi changamano kwa kurejelea vigezo vifuatavyo.

  • Muundo wa kawaida
  • Kundi nomino ambalo ni kapa.
  • Kundi tenzi ambalo lina kishazi tegemezi.
MUUNDO WA KAWAIDA

Mfano 1:

Miche iliyopandwa imekauka tena.

iliyopandwa’ ni kishazi tegemezi,kwa hivyo, ‘miche iliyopandwa’ ni kundi nomino (zingatia miundo ya kundi nomino), ‘imekauka tena’ ni kundi tenzi.

Uchanganuzi

uchanganuzi

Mfano 2:

Mtoto wao aliyepotea jana amepatikana barabarani.

aliyepotea jana’ ni kishazi tegemezi,kwa hivyo, ‘mtoto wao aliyepotea jana’ ni kundi nomino (zingatia miundo ya kundi nomino), ‘amepatikana barabarani’ ni kundi tenzi.

Uchanganuzi

uchanganuzi

KUNDI NOMINO AMBALO NI KAPA

Mfano 3 :

Vilivyonunuliwa vitapakwa rangi.

Katika makala yaliyotangulia tuliona kuwa sentensi ya Kiswahili huwa na sehemu mbili kuu,kundi nomino na kundi tenzi,lakini kundi nomino huweza kuondolewa na maana ya sentensi ikaifadhiwa.

Hatujui ni vitu gani vilivyopakwa rangi,kundi nomino hapa ni kapa.Vilevile,neno ‘vilivyonunuliwa’ ni kashazi kinachovumisha nomino fulani ambayo haijatajwa.

Uchanganuzi

uchanganuzi

KUNDI TENZI LENYE KISHAZI TEGEMEZI

Kishazi tegemezi huweza kujitokeza katika kundi tenzi,mara nyingi kinatumika kama kielezi.

Mfano 4:

Mjomba alishtuka alipopigiwa simu.

alipopigiwa simu’ mi kishazi tegemezi, kinafafanua zaidi kitendo cha kushtuka, ‘alishtuka alipopigiwa simu’ ni kundi tenzi(zingatia miundo ya kundi tenzi)

Uchanganuzi

uchanganuzi

      Lesson Video     

 

Content Protection by DMCA.com
Share this;
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ibrah
Ibrah
3 months ago

Asante