Umuhimu wa mhusika

Swali la Dondoo: Kigogo

“Jina lako litashamiri. Utapata tuzo nyingi pia”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Fafanua umuhimu wa msemaji wa kauli hii katika tamthilia. (alama 8)

c) Eleza mbinu zingine anazotumia Majoka kuongoza Sagamoyo. (alama 8)

Majibu

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Vigezo katika kueleza Umuhimu wa Mhusika

Swali la kujadili umuhimu wa mhusika fulani ni rahisi iwapo mwanafunzi anakumbuka mtiririko wa matukio vizuri. Ikumbukwe kuwa swali hili hutolewa mifano pia. Mtahiniwa anaweza kuzingatia vigezo vifuatavyo;

 1. Je, mhusika huyu ametumiwa kupitisha maudhui gani?
 2. Je, mhusika huyu ametumiwa kuonyesha sifa za wahusika wengine?
 3. Je, ametumika katika kuendeleza ploti?
 4. Je, anawakilisha watu wa aina gani katika jamii? Kwa mfano, Majoka anawakilisha viongozi ambao ni wakatili katika jamii
 5. Je, ametumiwa kama kielelezo cha kina nani katika jamii? Kwa mfano, watetezi wa haki.
 6. Je, anaibua mambo gani katika jamii? Kwa mfano, Katika hadithi “Mkubwa” Mkumbukwa anaonyesha changamoto wanazoipitia mahabusu……
Content Protection by DMCA.com
Share this;
kigogo

Swali la Dondoo: Kigogo

Tamthilia ya Kigogo-Pauline Kea

“Ameenda kutafuta kiamshakinywa”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

Haya ni maneno ya Sudi kwa Tunu.Wako barazani mwa nyumba ya Sudi.Ni baada ya Pili kuitisha chakula kwani ana njaa. Tunu anataka kujua alikoenda Ashua. (4×1)

b) Fafanua umuhimu wa anayerejelewa na kauli hii. (alama 8)

 • Ashua ametumiwa kuonyesha wanawake ambao ni waaminifu katika ndoa. Anakataa kushiriki mapenzi na majoka.
 • Ni kielezi cha wanawake ambao ni walezi wema. Anaenda kuwataftia watoto wake chakula baada ya soko kufungwa.
 • Ni mfano wa watu ambao ni wasomi katika jamii. Ashua amesoma na kuhitimu kama mwalimu.
 • Ametumiwa kuendeleza maudhui ya uongozi mbaya. Kupitia kwake tunaona taabu wanazopitia wanasagamoyo baada ya soko kufungwa.Wanakosa chakula.
 • Ametumiwa kuonyesha nafasi ya mwanamke katika jamii. Wanawake ni chombo cha mapenzi.Majoka anataka kushiriki mapenzi na ashua ili ampe msaada.
 • Ametumiwa kuendeleza maudhui ya dawa za kulevya. Kupitia kwake tunatambua kuwa wanafunzi katika shule ya Majoka and Majoka academy hawafunzu,wamegeuka makabeji kwa kutumia sumu ya nyoka.
 • Ni kielelezo cha wanawake wenye bidii. Ingawa hajapata kazi anauza maembe sokoni chapakazi ili kupata riziki.

c) Huku ukitoa maelezo onyesha wahusika wengine wanne wanaompinga msemewa. (alama 8)

 • Ngurumo- huyu ni mfuasi sugu wa Majoka.Anasema hawezi kumpigia kura Tunu.
 • Majoka- huyu ni kiongozi wa sagamoyo. Yeye na Majoka wanapanga jama ya kumkomesha Tunu. Wanamtuma Chopi na vijana wengine kuenda kumwangamiza Tunu.
 • Kenga- huyu ni mshauri mkuu wa majoka. Anasema kuwa lazima waweke kina Tunu vidhibiti mwendo na hatimaye kuwakomesha kabisa.
 • Chopi- ni mlinzi wa majoka, alitumiwa na majoka na kenga kumkomesha Tunu, walipewa amri ya kumwangamiza ingawa walimvunja mguu.

Maswali zaidi


Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat