silabi

pronunciation

Aina na miundo ya silabi

Silabi ni kipashio kinachotamkika

Maana

Sauti mbili au zaidi zinazotamkwa kwa pamoja.

Sauti mbili au zaidi ambazo hutamkwa kama  fungu moja la sauti.

Aina za silabi

Kuna aina mbili za sila katika Kiswahili

Silabi funge

Hizi ni silabi ambazo huishwa kwa konsonanti

Mfano: Lab-da

Silabi wazi

Hizi ni silabi ambazo huishia kwa irabu

Mfano: ka-ka, le-o,u-si-ku

MUUNDO WA SILABI

Kuna miundo mbalimbali ya silabi katika Kiswahil

Irabu pekee

o-a,i-ta

konsonanti pekee

m-tu

konsonanti irabu

ji-tu

konsonanti konsonanti irabu

mje-ngo,msi-tu

konsonanti konsonanti konsonanti irabu

mbwe-ha,twa-ngwa

Mifano ya maswali

 1. Eleza maana ya silabi.(alama 1)
 2. Huku ukitoa mifano eleza aina mbili za silabi. (alama 2)
 3. Eleza miundo yoyote miwili ya silabi. (alama 2)
 4. Tenganisha silabi: viyeyusho  (alama 2)
 5. Tunga neno lenye muundo ufuatao: KI+KI+I. (alama 2)
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Dhana ya mofimu

Mofimu

Karibuni katika kipindi cha leo ili tujifunze aina, mifano na matumizi ya mofimu katika lugha ya Kiswahili.


Mofimu ni nini?

Mofimu ni kipashio kidogo katika lugha ambacho hakiwezi kugawika zaidi bila kupoteza maana yake ya kisarufi.

Tofauti ya Kiambishi na Mofimu

Ikumbukwe kuwa kiambishi ni mofimu ambayo huongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuwakilisha dhana fulani.Pia,kiambishi hujitokeza kama mofimu tegemezi. Tofauti kuu hapa ni kuwa mofimu huweza kujisimamia kiimaan(mofimu huru) ilhali kiambishi hutegemea viambishi vingine ili kukamilisha maana.

Sifa za Mofimu

Kutokana na maelezo haya tunaweza kuorodhesha sifa zifuatazo za mofimu.


1.Mofimu ni kipashio chenye maana ya kisarufi.

Ni kweli kuwa mofimu hubeba maana ya kisarufi. Vijisehemu hivi ni muhimu sana katika sarufi.

Kwa mfano, katika neno anacheka tunaweza kupata mofimu zifuatazo.

a-na-chek-w-a

Mofimu                                   Maana ya kisarufi

a                                              nafsi ya tatu umoja

na                                           wakati uliopo

chek                                         mzizi

w                                             kauli/mnyambuliko wa kitenzi

a                                              kauli tenda/kiishio


 1. Mofimu haiwezi kugawika zaidi

Mofimu tulizoziona hapo juu haziwezi kuvunjwavunjwa zaidi. Zitapoteza maana.

Ni vizuri kutofautisha silabi na mofimu.

Silabi ni kipashio cha utamkaji ilhali mofimu ni kipashio kidogo cha kisarufi chenye maana.

Kwa hivyo,tunapoonyesha mofimu katika neno tuwe makini tusionyeshe silabi.

Tazama neno lifuatalo: Anaimba

Silabi: a+na+i+mbi+wa

Silabi hutamkika,vilevile baadhi ya vijisehemu hivi havina maana ya kisarufi.

Mofimu: a-na-imb-iw-a

Sehemu hizi zina maana ya kisarufi.

Aina mbili kuu za mofimu

 1. Mofimu huru
 2. Mofimu tegemezi

Mofimu huru

Mofimu huru hujisimamia kimaana kama neno kamili.Kimsingi hili ni  neno kamili kwa sababu lina maana iliyokamilika. Haliwezi kuvunjavunjwa bila kupoteza maana yake.

Mfano: leo,simu,meza,peremende,karatasi,darasa,hukumu,jaji,picha …

TANBIHI: Maneno haya yanaweza kuambishwa na kuwa mofimu tegemezi.

Mfano: jimeza (ji+meza)


Mofimu tegemezi

Hii ni mofimu ambayo hutegemea mofimu nyingine ili kuleta maana inayokusudiwa.

Mfano ;

Mtu : m-tu,wa-tu

Komesha: kom-esh-a

Letwa : let-w-a


Majukumu ya mofimu katika neno

 1. Mzizi wa neno

Mzizi unaweza kuwa huru au funge

Mzizi huru: sahau,dharau,safiri

Mzizi funge: fung,pik,som,chek,l,ny,ch


 1. Nafsi
NAFSI UMOJA WINGI vitenzi
Ya kwanza NI TU ni-na-ok-a, tu-na-ok-a
Ya pili U M u-na-ok-a, m-na-ok-a
Ya tatu A WA a-na-ok-a, wa-na-ok-a

 1. Ngeli

a-na-li-a : a-ngeli ya A-WA

li-me-fik-a: li-ngali ya LI-YA


 1. Umoja na wingi

m-tu: m-umoja

wa-tu: wa-wingi

ma-toto: ma-wingi


 1. Hali

Me-hali timilifu-amechoka

Hu- hali ya mazoea-hucheza

a-Hali isiyodhihirika-akamatwa

po- hali ya mazoea/wakati wowote- asomapo

ki-hali ya masharti- akija


 1. Yambwa (mtendwa/shamirisho kipozi, mtendewa/yambiwa/shamirisho kitondo)

Ku- nitakuonyesha

m-nitampigia

wa-nitawakomesha


 1. Mahali

Po- aliposimama (matumizi ya po mara nyingi hujitokeza kimuktadha)

Ni –kanisani,dukani,bungeni

Ko-alikoingia

Mo-alimoingia


 1. Kiulizi

Wasemaje?

 1. Amri

Ni- someni,simameni,tokeni


 1. Kauli/mnyambuliko

Mofimu za kauli za vitenzi ni nyingi sana katika lugha ya Kiswahili.

Kwa mfano:

a-Kauli tenda: fik-a

w-kauli tendwa: som-w-a

liw-kauli tendewa: kagu-liw-a

ek-kauli tendeka: pik-ik-a

esh-kauli tendesha: wez-esh-a


 1. Vikanushi

Ku-kikanushi cha wa wakati uliopita : hakusoma

Ja-kikanushi cha hali timilifu: hajakuona

Si-kikanushi cha nafsi ya kwanza: siendi

Hu-kikanushi cha nafsi ya pili: huendi

Ha-kikanushi cha nafsi ya tatu: haendi

Namna ya kutambua mofimu za  kukanusha

Andika neno katika hali yakinifu kisha ulikanushe

Anasoma- hasomi

Amesoma-hajasoma

 Alisoma-hakusoma


 1. Kijalizo

Ku-alikuja


 1. Kiishio/kauli tenda

A:chek-a


 1. Ukubwa na udogo wa nomino

Ki-udogo: kitoto

Ji-ukubwa:jitoto


Maswali

 1. Eleza maana ya mofimu. (alama 1)
 2. Tofautisha mofimu na kiambishi. (alama 1)
 3. Tofautisha mofimu huru na mofimu tegemezi. (alama 2)
 4. Toa mifano miwili ya mofimu huru. (alama 1)
 5. Bainisha mofimu katika neno lifuatalo; (alama 3) Hatujajibiwa
Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat