sentensi

alama ya kishazi tegemezi

Uchanganuzi wa Sentensi Changamano : Kielelezo cha Jedwali

Utangulizi

Sentensi changamano huwa na kishazi huru na kishazi tegemezi. Rejelea makala kuhusu aina za sentensi kimuundo pamoja na aina za uchanganuzi wa sentensi. Makala ya leo yatashughulikia kielelezo cha jedwali.

Hatua za uchanganuzi

 1. Tambua kundi nomino na kundi tenzi
 2. Tambua kishazi tegemezi.Je,kishazi tegemezi kinajitokeza upande wa kundi nomino au kundi tenzi ?
 3. Tambua aina mbalimbali za maneno

Mfano 1

Runinga iliyonunuliwa ni ya jirani.

Kishazi tegemezi : iliyonunuliwa

                                                  S
                 KN   KT
          N t H N
Runinga iliyonunuliwa ni ya jirani

Mfano 2

Kijana huyo anayekupigia simu alifika jana.

Kishazi tegemezi: anayekupigia simu

                                                  S
                 KN   KT
         N V   T E
Kijana huyo anayekupigia simu alifika jana

Mfano 3

Dola alilicheka alipoanguka sakafuni

Kishazi tegemezi: alipoanguka sakafuni

                                                             S
KN                          KT
N T
Dola alicheka alipoanguka sakafuni

Mfano 4

Askari ambaye alimkamata ni mwadilifu

Kishazi tegemezi: ambaye alimkamata

                                                         S
               KN                          KT
N t V
Askari ambaye alimkamata ni mwadilifu

Maswali

Changanua sentensi zifuatazo kwa kielelezo cha jedwali

 1. Hiyo siku aliyokutembelea alikaribishwa vizuri.
 2. Mfanyikazi alifurahi aliponunuliwa zawadi.
 3. Pili ambaye alipita mtihani ni mwanafunzi mwenye bidii.
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Sentensi Ambatano

MAANA : Sentensi ambatano ni sentensi ambayo ina vishazi huru viwili au zaidi.

Kishazi huru huwa na maana kamili. Kikiondolewa katika sentensi kuu huwa kina maana iliyokamilika.

Mara nyingi sentensi ambatano  huwa na kiunganishi. Kiunganishi hiki hutumiwa kuziunganisha vishazi hivi. Hivyo basi, sentensi ambatano huwa na sentensi mbili au zaidi ambazo zimekamilika kimaana na kuunganishwa pamoja.

Mifano 1

 Mhuburi anahubiri na watoto wanalia kanisani

Sentensi hii ina vishazi huru viwili

 • Mhubiri anahubiri.
 • Watoto wanalia kanisani

Mifano zaidi

 1. Anapiga simu lakini mteja hapatikani.
 2. Anacheza huku akicheka.
 3. Ametumwa bungeni na rais ili kupitisha ujumbe wa dharura.
 4. Daktari huyu hutibu wagonjwa vizuri lakini yule ana mzaha kazini.

Kama ilivyo katika sentensi zingine, sentensi ambatano pia inaweza kuchanganuliwa kwa kutumia njia zifuatazo.

 1. Kistari
 2. Mishale
 3. Jedwali
 4. Matawi

Tuangalie uchanganuzi wa sentensi ambatano kwa njia ya kistari

Mhuburi anahubiri na watoto wanalia kanisani

S———-S1+U+S2

S1——–KN+KT

KN——-N

N——–mhubiri

KT——- T

T——— anahubiri

U——– na

S2———KN+KT

KN——–N

N———- watoto

KT———T+E

T——–wanalia

E——– kanisani

Anacheza huku akicheka.

S———–S1+U+S2

S1———-KN+KT

KN———ø

KT———-T

T———- anacheza

U———- huku

S2———–KN+KT

KN——— ø

KT———-T

T———— akicheka

Content Protection by DMCA.com
Share this;
alama ya kishazi tegemezi

Sentensi Ambatano Changamano

Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu sentensi ambayo ni ambatano lakini ina kishazi tegemezi! Ikumbukwe kuwa sentensi huainishwa kimuundo kwa kuzingatia vishazi.

Kimuundo kuna aina tatu za sentensi katika lugha ya Kiswahili

Ambatano Changamano

Sentensi ambatano changamano  ina vishazi huru viwili au zaidi pamoja na kishazi tegemezi

Tazama sentensi ifuatayo

Rais aliyechaguliwa anawahutubia wananchi  lakini wote wanapiga kelele

S1: Rais aliyechaguliwa anawahutubia wananchi

S2: wote wanapiga kelele

U: lakini

Kishazi tegemezi: aliyechaguliwa

Uchanganuzi

                                                                S
                  S1 U                    S2
KN     KT  

lakini

KN KT
N T N W T N
Rais aliyechaguliwa anawahutubia wananchi wote wanapiga kelele

 

Kimsingi hii ni sentensi ambatano lakini ndani yake kuna kishazi tegemezi.

Mifano zaidi

Mtoto ambaye analia ni wetu lakini sisi sote tutamsaidia.

 

 

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Aina za maigizo katika Fasihi Simulizi

waigizaji

AINA ZA MAIGIZO

Makala haya yanafafanua aina kuu za maigizo, wala si vipera vya maigizo

Maigizo ni utanzu muhimu sana katika Fasihi Simulizi. Watendaji huweza kuiga tabia za wahusika wengine ili kuwasilisha ujumbe fulani katika jamii. Utanzu huu una vipera mbalimbali kama vile, vichekesho na michezo ya jukwaani.

Leo nitazungumzia aina mbili kuu za maigizo. Aina ni tofauti na vipera. Maigizo yamegawika katika aina mbili kuu ambazo ni;

 1. Sanaa ya maonyesho.
 2. Maigizo ya kawaida.
 1. SANAA YA MAONYESHO

Sanaa ya maonyesho huashiria matendo ya kweli katika jamii. Matendo haya ni kama vile miviga ambayo imekuwepo tangu jadi. Mambo haya  huongozwa na itikadi fulani za jamii husiika.Kama ilivyo katika aina nyingine ya maigizo,sanaa ya maonyesho hujumuisha hadhira ambayo mara nyingi huwa watendaji.

Ikumbukwe kuwa sanaa ya maonyesho hujikita katika kuendeleza mila na desturi za jamii,si kuburudisha tu. Waandishi wengi wamefafanua dhana hii kwa njia nyingi tofauti,kunao wanaeleza sanaa ya maonyesho kama kipera cha maigizo,wengine wanayaweka maigizo chini ya sanaa ya maonyesho.

Kitendo cha kuigiza huenda ata kisijitokeze moja kwa moja,kwa mfano tendo la kusalia miungu katika jamii za Kiafrika. Kwa kweli ,si rahisi kueleza mipaka iliyopo kati ya sanaa ya maonyesho na maigizo.

Shuguli hizi na matendo yake huwa ya kweli yanapofanyika katika mazingira halisi ya  jamii fulani, kwa mfano matambiko.

Kutokana na maelezo haya tunaweza kupata sifa zifuataza za sanaa ya maonyesho

 • Hakuna haja ya jukwaa
 • Hakuna vifaa maalumu.
 • Hufanyika wakati maalumu kulingana na utamaduni wa jamii husika.
 • Wanaoshiriki utendaji huu hawaitaji kufanya mazoezi kabla ya utendaji wenyewe.
 • Watendeji huweza kuwa hadhira pia.
 • Utendaji huonyesha mambo halisi na ya kweli katika jamii.
 • Kimuundo utendaji hufululizwa kutoka mwanzo hadi mwisho

 Download my ebook

 1. MAIGIZO YA KAWAIDA

Maigizo ya kawaida hutambulika kwa haraka. Kwa mfano,michezo ya jukwaani. Watendaji hujitayarisha kabla ya kuenda mbele ya hadhira. Baadhi ya vipera katika kitengo hiki havikuwepo katika jamii za Kiafrika. Vinahusishwa na kuja kwa Wakoloni. Maigizo haya pia huweza kuingiliana na Fasihi Andishi kwa sababu huwa kuna maandishi kwanza, kama vile tamthilia au riwaya ambayo wahusika huisoma kabla ya kuigiza mbele ya hadhira maalumu.

Kuna sifa nyingi za maigizo ya kawaida

 • Kuna wahusika maalumu.
 • Matukio huwa ya kuiga, si ya kweli.
 • Huweza kufanyika wakati wowote.
 • Kuna hadhira maalumu
 • Hutumia vifaa maalumu ili kuwakilisha mazingira fulani.
 • Hufanyika wakati wowote
 • Kuna jukwaa maalumu.

SWALI

Linganisha na ulinganue sanaa ya maonyesho na maigizo ya kawaida.

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Maana ya sentensi sahili

Sentensi ni neno au kifungu cha maneno chenye ujumbe kamili.

Katika lugha ya Kiswahili kuna aina tatu za sentensi kimuundo.

Leo tutazungumzia sentensi sahili.Sentensi sahili huwa na kishazi huru kimoja,kwa hivyo inaeleza dhana moja tu.Inaweza kuwa hata na neno moja tu.

Kwa mfano: Wamewasili.

“Wamewasili” ni sentensi kamili.Inapitisha ujumbe na ina sehemu kuu za sentensi,yaani,kiima na kiarifu.

Mara nyingi sentensi sahili huwa na kitenzi kimoja.

 1. Serikali imezindua mbinu mpya za ukulima.
 2. Wakenya kulalamikia sheria mpya.

Hata hivyo,kuna uwezekano wa kuwa na vitenzi viwili au zaidi.Hivi ni vitenzi visaidizi pamoja na kitenzi kikuu.

1.Serikali ilikuwa imezindua mbinu mpya za ukulima.

2.Wakenya wangali wanalalamikia sheria mpya.

Kama ilivyo katika sentensi zingine,sentensi sahili huwa na kundi nomino na kundi tenzi.Iwapo ni sentensi ya neno moja,kundi nomino huwa kappa.

Kwa kutamatisha: Sentensi sahili ni sentensi yenye wazo moja tu. Vilevile huwa na kishazi kimoja ambacho ni kishazi huru.

Maswali.

 1. Eleza maana ya sentensi sahili.
 2. Tunga sentensi sahili.
 3. Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo.

Nyumba kubwa sana inajengwa mjini.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat