methali

Methali Tamu za Kiswahili

Top 10 Swahili proverbs

 • Haraka haraka haina Baraka
  • Ukifanya jambo kwa haraka huenda usifanikiwe
 • Mke ni nguo mgomba ni kupalilia
  • Kitu kizuri huwa kimetunzwa vizuri
 • Chelewa chelewa utapata mwana si wako
  • Mtu ambaye huwa wa kwanza katika jambo huweza kupata kitu kizuri
 • Masikini akipata matako hulia mbwata
  • Mtu ambaye alikuwa mhitaji akifanikiwa huanza kuwa na maringo
 • Adui wa mtu ni mtu
  • Adui wa mtu ni mtu
 • Maskini haokoti akiokota huambiwa kaiba
 • Mtu ambaye ni maskini hukosa mafanikio katika mambo mengi maishani
 • Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni
  • Ukishangazwa na jambo moja kuna jambo jingine kubwa zaidi na litakushangaza zaidi
 • Angurumapo samba mcheza nani?
  • Mtu mwenye uwezo/mamlaka akiongoea wengine hunyamaza
 • Akili nyingi huondoa maarifa
  • Iwapo mtu anajiona mwerevu sana huenda akaanza kufanya upumbavu
 • Akili ni nywele kila mtu ana zake
  • Kila mtu ana uwezo/busara/maarifa ya kufanya jambo Fulani
 • Mgeni njoo mwenyeji apone
  • Mgeni ni Baraka kwa mwenyeji
 • Siku za mwizi ni arubaini
  • Maovu huwa na mwisho wake
 • Mwizi akishikwa husema kaokota
  • Mtu akifanya jambo baya hutafuta kisingizio ili kujitetea
 • Mgema akisifiwa tembo hulitia maji
  • Sifa nyingi zinaweza kumpotosha mtu
 • Usimwage mtama kwenye kuku wengi
  • Usiwe na tabia ya kutoa siri zako mbele ya watu wengi
 • Wema hauozi
  • Matendo mazuri huleta faida
 • Ngoja ngoja huumiza matumbo
  • Kuchelewa kutekeleza jambo Fulani husababisha madhara
 • Siku ya nyani kufa miti yote huteleza
  • Ujanja/unafiki/Maovu ambayo mtu amekuwa akifanya siku ya kugunduliwa ikifika hana pa kujificha
 • Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kusonga ugali.
  • Ata ukipatwa na changamoto maishani usife moyo
 • Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga
  • Ukifanya jambo baya itakubidi ukubali matokeo yake
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Methali ya Leo

Methali: Ajizi ni nyumba ya njaa


Ajizi : uzembe/uvivu

Maana: uvivu husababisha njaa

Matumizi: Methali hii inaweza kutumiwa kwa mtu ambaye analalamika kuwa ana taabu/njaa ingawaje yeye ni mvivu.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat