matumizi ya lugha

a unganifu

Matumizi ya a-unganifu

UAMILIFU WA A-UNGANIFU

A-unganifu huwa na matumizi mbalimbali katika lugha ya Kiswahili.

Sehemu hii katika sentensi huunda kirai kihusishi kwani neno kuu huwa ni kihusishi

Mfano

 1. Nyumba ya mbao
 2. Kiti cha enzi.
 3. Gari la abiria.

Sehemu zilizopigiwa mstari ni kirai kihusishi

Aghalabu, kihusishi <a> hufuatwa na nomino.

Matumizi ya a- unganifu

Kuonyesha aina ya kitu/jambo fulani

 1. Chumba cha malazi
 2. Dawa za malaria.
 3. Maji ya mto.
 1. Uwanja wa ndege.
 2. Mashairi ya arudhi

Kuonyesha umilikaji

 1. Kitabu cha mwanafunzi.
 2. Mali ya umma.
 3. Gari la rais.

Kuonyesha nafasi katika orodha

 1. Waziri wa kwanza kufiki bungeni ni yupi ?
 2. Kipchoge amemaliza akiwa wa nne.
 3. Mtahiniwa wa tatu amefika.

Swali

Tunga sentensi yenye kirai kihusishi kinachoonyesha nafasi katika orodha.(alama 2)

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Maana ya sentensi sahili

Sentensi ni neno au kifungu cha maneno chenye ujumbe kamili.

Katika lugha ya Kiswahili kuna aina tatu za sentensi kimuundo.

Leo tutazungumzia sentensi sahili.Sentensi sahili huwa na kishazi huru kimoja,kwa hivyo inaeleza dhana moja tu.Inaweza kuwa hata na neno moja tu.

Kwa mfano: Wamewasili.

“Wamewasili” ni sentensi kamili.Inapitisha ujumbe na ina sehemu kuu za sentensi,yaani,kiima na kiarifu.

Mara nyingi sentensi sahili huwa na kitenzi kimoja.

 1. Serikali imezindua mbinu mpya za ukulima.
 2. Wakenya kulalamikia sheria mpya.

Hata hivyo,kuna uwezekano wa kuwa na vitenzi viwili au zaidi.Hivi ni vitenzi visaidizi pamoja na kitenzi kikuu.

1.Serikali ilikuwa imezindua mbinu mpya za ukulima.

2.Wakenya wangali wanalalamikia sheria mpya.

Kama ilivyo katika sentensi zingine,sentensi sahili huwa na kundi nomino na kundi tenzi.Iwapo ni sentensi ya neno moja,kundi nomino huwa kappa.

Kwa kutamatisha: Sentensi sahili ni sentensi yenye wazo moja tu. Vilevile huwa na kishazi kimoja ambacho ni kishazi huru.

Maswali.

 1. Eleza maana ya sentensi sahili.
 2. Tunga sentensi sahili.
 3. Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo.

Nyumba kubwa sana inajengwa mjini.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat