kutambua sifa za wahusika

Vigezo katika kueleza Umuhimu wa Mhusika

Swali la kujadili umuhimu wa mhusika fulani ni rahisi iwapo mwanafunzi anakumbuka mtiririko wa matukio vizuri. Ikumbukwe kuwa swali hili hutolewa mifano pia. Mtahiniwa anaweza kuzingatia vigezo vifuatavyo;

 1. Je, mhusika huyu ametumiwa kupitisha maudhui gani?
 2. Je, mhusika huyu ametumiwa kuonyesha sifa za wahusika wengine?
 3. Je, ametumika katika kuendeleza ploti?
 4. Je, anawakilisha watu wa aina gani katika jamii? Kwa mfano, Majoka anawakilisha viongozi ambao ni wakatili katika jamii
 5. Je, ametumiwa kama kielelezo cha kina nani katika jamii? Kwa mfano, watetezi wa haki.
 6. Je, anaibua mambo gani katika jamii? Kwa mfano, Katika hadithi “Mkubwa” Mkumbukwa anaonyesha changamoto wanazoipitia mahabusu……
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Namna ya kutambua sifa za wahusika katika fasihi

 1. Maelezo ya mwandishi

Waandishi mara nyingi hutaja sifa za wahusika moja kwa moja au kwa njia ya maelezo.

Shogake Dada ana Ndevu-Alifa Chokocho

Safia

Ni mwenye bidii- hachoki kumsaidia mamake kazizi yoyote mle nyumbani mwao,hupika,huosha vyombo,hufua ,hupiga pasi na kutandika kila siku.

Ni mcha mungu- anafuata kanuni zote alizoamrisha Mungu kupitia dini yao.

Tumbo Lisiloshiba- Said A.Mohamed

Mzee Mago

Ni mtetezi  wa haki-yeye hupiga mbio huku na kule ,kujaribu hili na lile,kuzuia haki isiangamizwe.

Ni mwenye ushawishi-anawaleta Wanamadongoporomoka pamoja kupigania haki ya kuishi Madongoporomoka.

Mapenzi ya Kifaurongo- Kenna Wasike

Penina

Ni mnafiki- anamwambia Dennis kwamba anampenda licha ya umaskini wake.Baadaye anamgeuka, “potelea mbali mkata wee!”

 1. Majina ya wahusika

Wahusika katika Fasihi hupewa majina ya kimajazi.Majina haya hutusaidia kutambua tabia na sifa zao.

Shogake Dada ana Ndevu- Alifa Chokocho

Kutoka na neno safi tunaelekea kutambua kuwa Safia ni mhusika  mwenye sifa nyingi chanya.NI msaidizi wa wazazi wake,ni mwenye bidii,ni hodari shuleni na ni mcha mungu.

Tamthilia ya Kigogo- Pauline Kea

Boza– boza ni mtu mpumbavu. Mhusika huyu anawaunga mkono Majoka na Kenga ingawaje hawajali maslahi yake. Wanafunga soko anakofanyia kazi, anaunga mkono sherehe za mwezi za kusherehekea uhuru  ilhali hawana cha kusherehekea, haki zao zinakiukwa na hawana chakula.

 1. Matendo ya wahusika

Tumbo Lisiloshiba- Said A.Mohamed

Jitu la miraba minne

Ni lenye ulafi- linakula chakula kingi na halishibi.

Ni lenye tamaa- linamwambia Mzee Mago kuwa limekuja kula ardhi yake.Lina hamu kubwa kupata ardhi ya Wanamadongoporomoka.

Mapenzi ya Kifaurongo- Kenna Wasike

Dennis

Ni mwenye bidii- ametoka katika familia maskini lakini anajitahidi hadi kufaulu masomoni.

Ni mwenye mapenzi ya kweli- anampenda Penina licha ya tofauti ya matabaka.Anampeleka Penina nyumbani kwao kwani wana mipango ya kuoana.

 1. Mazungumzo baina ya wahusika

Kutokana na namna mtu anavyozungumza unaweza kueleza sifa ningi kumhusu, mpyoro,mwenye kiburi na kdh.

Tumbo Lisiloshiba- Said A.Mohamed

Jitu la miraba minne

Ni lenye kiburi- linamwambia Mzee Mago, “mimi sitaki naam zako nyingi wala sitaki msaada wako dhaifu.

 1. Namna mhusika anavyosema kumhusu mhusika mwingine

Mhusika anaweza kutaja sifa ya mhusika mwingine moja kwa moja au kwa njia ya maelezo.

Mame Bakari- Mohammed Khelef Ghassany

Babake Sara

Ni mkaidi-  “Bwana yule mwenye masikio makaidi na mwenye tabia ya kutoamini maafa ya mtu mwengine?”

Ni mkali – “ angelipasuka kwa ukali tu”

Haya ni maneno ya mhusika Sara

 1. Namna wahusika walivyovalia

Mavazi ya wahusika pia ni muhimu katika kutambua sifa za wahusika na umuhimu wao katika fasihi.

Shogake Dada ana Ndevu- Alifa Chokocho

Kimwana

Ni mwongo- anaingia kwa kina Safia akiwa amevaa buibui ilhali yeye ni mwanamume.

SWALI

Je, unatambua nini kutokana na mavazi ya wahusika hawa katika tamthilia ya Kigogo na Pauline Kea?

 • Ashua (katika soko la chapakazi)
 • Husda (Majoka and Majoka modern Resort)
Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat