kinaya katika kigogo

Swali la Dondoo: Kigogo

“Sina muda wa kufikiria mambo ya watu…nafikiria maneno matamu kama asali”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

majibu
b) Tambua mbinu ya kimtindo iliyotumika katika dondoo hili. (alama2)

majibu
c) Fafanua sifa zozote sita za msemewa katika kauli hii. (alama 6)

majibu
d) Jadili maudhui ya unafiki kama yanavyojitokeza katika tamthilia hii. (alama 8)

Tazama Majibu

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Majibu: Swali la Dondoo

MAJIBU
“Sina muda wa kufikiria mambo ya watu…nafikiria maneno matamu kama asali”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

i. Maneno ya Majoka
ii. Msemewa ni Chopi
iii. Mahali ni Majoka and Majoka Modern Resort
iv. Majoka amefahamishwa kifo cha Ngurumo na Chopi ni kusema afukiwe juu ya wengine.
v. Majoka ametoa amri kuwa chatu mmoja atolewe kafara ili wakereketwa wa mazingira waanze kuandamana hivyo basi kamera hazitaelekezwa makaburini

b) Fafanua sifa zozote sita za msemewa katika kauli hii. (alama 6)

i. Mtiifu/mwaminifu – anamheshimu Majoka na kufuata amri zake kikamilifu.Alifuata amri ya kumkamata Ashua.
ii. Mkatili– alishiriki katika kumvunja Tunu mguu. Alikuwa amepewa amri ya kumwangamiza.
iii. Ni mpyoro– anamwita Sudi ngiri
iv. Ni kikaragosi– anatumiwa na Majoka kuendeleza utawala wa kidhalimu. Anahusika katika kumvamia Tunu na kumvunja mguu kwani Tunu anapinga uongozi wa Majoka.
v. Ni mwenye kiburi– anamkemea Sudi na kumwambia atoke katika chumba cha wafungwa na iwapo ameshindwa kumtunza Ashua amwambie.
vi. Ni mslati – walinzi wa Majoka wanapomwona Kingi akibebwa na kushangilia na umati wanaacha kumlinda Majoka.Chopi ni mlinzi wa Majoka.

c) Onyesha kinyume kinachojitokeza katika kauli hii. (alama 2)
Majoka anasema hana muda wa kumfikiria Ngurumo ilhali alikuwa mfuasi wake

d) Fafanua matumizi mengine ya mbinu hii katika tamthilia (alama 8)

i. Ni kinaya kuwa serikali ya Majoka inakusanya kodi lakini soko ni chafu.
ii. Sudi anasema kuwa serikali ya majoka inachukua kilicho chao na kuwatisha.
iii. Katinga matangazo ya redio wanasagamoyo wanatangaziwa kipindi cha mwezi mmoja cha kusherehekea ufanisi wao- hakuna ufanisi Sagamoyo,soko ni chafu,kuna maandamano na watawaliwa kutishwa.
iv. Ngurumo ni mfuasi sugu wa Majoka lakini anapokufa Majoka anasema afukiwe juu ya wengine na hana muda wa kufikiria mambo ya watu.
v. Chopi ni mwaminifu kwa Majoka lakini aliposhindwa kumwangamiza Tunu Kenga na Majoka wana njama ya kumwangamiza.
vi. Ngurumo anasema kuwa pombe inawapa starehe lakini kuna watu wamekuwa vipofu.
vii. Kenga anamwambia Majoka aache moyo wa huruma ingawaje Majoka anatoa amri ya kunyanyasa raia.Anasema atamkomesha Tunu.Pia,anamwambia Kingi awapige wananchi risasi.
viii. Boza anasema kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea ilhali mradi wa kuchonga kinyago umefadhiliwa kutoka nje.Pia wananchi hawana chakula,Ashua anaenda kwa Majoka kuomba chakula.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    Open chat