fasihi simulizi

Mbinu za Kukusanya Fasihi Simulizi

Mbinu za Kukusanya Vitanza Ndimi {KCSE Kiswahili Paper 3 (102/3),Swali la lazima: 2013,}

Mbini hizi zinaweza kutumika katika ukusanyaji wa fasihi simulizi kwa jumla. Ufafanunuzi utategemea utanzu/kipera husika.

Utazamaji wa kushiriki au kutoshiriki.
Mtu anaweza kushiriki katika kikao cha utamkaji wa vitanza ndimi, hivyo kujua vinavyoendelezwa katika jamii husika.

Video
Mtu anaweza kupiga picha za video watu wakitamka/wakishindana katika utamkaji wa vitanza ndimi ili kuja kuchanganua baadaye.

Matumizi ya hojaji. Mtu anaweza kuandaa maswali katika hojaji ili kudadisi kwa mfano, kama vipo katika jamii fulani, wanaohusika katika vikao vya utamkaji na uundaji wake.

Kurekodi kimaandishi (kuandika) ili kuvirithisha au hata kuvichanganua
baadaye.

Majadiliano ya vikundi lengwa, Mtafiti anaweza kuteua vikundi, kwa mfano, vijana, ili kuchunguza namna wanavyoviunda na kuvitamka, na athari ya vitanza ndimi hivi kwao.

Mahojiano .Mtafiti anaweza kuandaa mahojiano rasmi na kundi / sampuli lengwa ili kuchunguza kwa mfano, majukumu ya vitanza ndimi katika jamii husika

Matumizi ya vinasa sauti ili kunasa utamkaji wenyewe na kuchanganua sifa zake.

Kutumia kumbukumbu ya mtafiti mwenyewe. Mtafiti ambaye in mmoja wa wanajamii katika eneo analofanyia utafiti anaweza kurithisha yale
anayokumbuka baada ya kuyashuhudia.

Kusoma majarida na vitabu (maktabani) vyenye habari kuhusu vitanza ndimi.

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Aina za maigizo katika Fasihi Simulizi

waigizaji

AINA ZA MAIGIZO

Makala haya yanafafanua aina kuu za maigizo, wala si vipera vya maigizo

Maigizo ni utanzu muhimu sana katika Fasihi Simulizi. Watendaji huweza kuiga tabia za wahusika wengine ili kuwasilisha ujumbe fulani katika jamii. Utanzu huu una vipera mbalimbali kama vile, vichekesho na michezo ya jukwaani.

Leo nitazungumzia aina mbili kuu za maigizo. Aina ni tofauti na vipera. Maigizo yamegawika katika aina mbili kuu ambazo ni;

 1. Sanaa ya maonyesho.
 2. Maigizo ya kawaida.
 1. SANAA YA MAONYESHO

Sanaa ya maonyesho huashiria matendo ya kweli katika jamii. Matendo haya ni kama vile miviga ambayo imekuwepo tangu jadi. Mambo haya  huongozwa na itikadi fulani za jamii husiika.Kama ilivyo katika aina nyingine ya maigizo,sanaa ya maonyesho hujumuisha hadhira ambayo mara nyingi huwa watendaji.

Ikumbukwe kuwa sanaa ya maonyesho hujikita katika kuendeleza mila na desturi za jamii,si kuburudisha tu. Waandishi wengi wamefafanua dhana hii kwa njia nyingi tofauti,kunao wanaeleza sanaa ya maonyesho kama kipera cha maigizo,wengine wanayaweka maigizo chini ya sanaa ya maonyesho.

Kitendo cha kuigiza huenda ata kisijitokeze moja kwa moja,kwa mfano tendo la kusalia miungu katika jamii za Kiafrika. Kwa kweli ,si rahisi kueleza mipaka iliyopo kati ya sanaa ya maonyesho na maigizo.

Shuguli hizi na matendo yake huwa ya kweli yanapofanyika katika mazingira halisi ya  jamii fulani, kwa mfano matambiko.

Kutokana na maelezo haya tunaweza kupata sifa zifuataza za sanaa ya maonyesho

 • Hakuna haja ya jukwaa
 • Hakuna vifaa maalumu.
 • Hufanyika wakati maalumu kulingana na utamaduni wa jamii husika.
 • Wanaoshiriki utendaji huu hawaitaji kufanya mazoezi kabla ya utendaji wenyewe.
 • Watendeji huweza kuwa hadhira pia.
 • Utendaji huonyesha mambo halisi na ya kweli katika jamii.
 • Kimuundo utendaji hufululizwa kutoka mwanzo hadi mwisho

 Download my ebook

 1. MAIGIZO YA KAWAIDA

Maigizo ya kawaida hutambulika kwa haraka. Kwa mfano,michezo ya jukwaani. Watendaji hujitayarisha kabla ya kuenda mbele ya hadhira. Baadhi ya vipera katika kitengo hiki havikuwepo katika jamii za Kiafrika. Vinahusishwa na kuja kwa Wakoloni. Maigizo haya pia huweza kuingiliana na Fasihi Andishi kwa sababu huwa kuna maandishi kwanza, kama vile tamthilia au riwaya ambayo wahusika huisoma kabla ya kuigiza mbele ya hadhira maalumu.

Kuna sifa nyingi za maigizo ya kawaida

 • Kuna wahusika maalumu.
 • Matukio huwa ya kuiga, si ya kweli.
 • Huweza kufanyika wakati wowote.
 • Kuna hadhira maalumu
 • Hutumia vifaa maalumu ili kuwakilisha mazingira fulani.
 • Hufanyika wakati wowote
 • Kuna jukwaa maalumu.

SWALI

Linganisha na ulinganue sanaa ya maonyesho na maigizo ya kawaida.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat