chozi la heri

Maudhui_Chozi la Heri

a) Wakimbizi hupitia matatizo mengi kambini. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea riwaya Chozi la Heri. (Alama 20)

b) Fafanua mchango mashirika yasiyo ya kiserikali katika jamii kwa kurejelea riwaya Chozi la Heri. (Alama 10)

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Maswali na majibu: Kigogo

Jamii imemkandamiza mwanamke.

Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea Tamthilia ya Kigogo.

1. Kudharauliwa

Majoka anasema wanawake ni wanawake tu.

2. Kutumiwa kama chombo cha mapenzi

Majoka anataka kuishiriki mapenzi na Ashua kama kigezo cha kumpa msaada.

3. Kupigwa

Tunu anapigwa na kuvunjwa mguu na Chopi,Ngurumo na vijana wengine.

4. Kutusiwa

Majoka anasema « sina time ya wanawake »

5. Kufungwa bila hatia

Majoka anamfunga Ashua kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali.Ilikuwa ni njia ya kulipiza kisasi kwa Sudi na kumnasa Ashua.

6. Kunyimwa kura

Tunu anapoenda mangweni kujaribu kuwakomboa walevi wamuimbia nyimbo za kumkejeli. Ngurumu anadai kuwa hawezi kumpa mwanamke kura.

7. Kutopewa nafasi ya uongozi katika jamii

Kenga anamwuliza Sudi iwapo Sagamayo ishawahi kuwa na Shujaa wa kike.

8. Kupangiwa njama ya kuuwawa

Kenga na Majoka wanapanga njama ya kumwangamiza Tunu.Wanawatuma vijana,akiwepo Chopi kumwangamiza lakini wanamvunja mguu.

9. Kuishi kwa hofu

Hashima anasema kuwa yeye na Tunu wake wanaishi kwa hofu,kila waamkapo wanapiga alhamdulillahi.

10. Kusalitiwa katika ndoa

Majoka anasema kuwa hampendi Husda bali alimwoa ili kutimiza wajibu wake kama kiongozi.Majoka anampenda Ashua.

Maswali mengine


Content Protection by DMCA.com
Share this;

Swali la Dondoo: Chozi la Heri

CHOZI LA HERI (ALAMA 20)

“…haifai kucheza na uwezo wa vijana,wao ni kama nanga.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)

c) Fafanua umuhimu wa msemaji wa kauli hii katika riwaya hii. (alama 8)

d) Onyesha namna vijana wanatumia uwezo wao katika riwaya hii. (alama 6)

Content Protection by DMCA.com
Share this;
chozi la heri cover page

Chozi la Heri: Swali la Dondoo (al 20)

Chozi la Heri: Assumpta Matei

Soma kauli ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuta

“ Sasa unarejea kwenu kupata tumekuporomosha kwa viganja vyetu wenyewe.”

a)   Eleza mukutadha wa dondoo hili. (alama 4)

b)   Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika kauli hii. (alama 2)

c)   Bainisha matumizi mengine kumi ya tamathali hii ya usemi katika riwaya. (alama 10)

d)   Huku ukitoa mifano katika riwaya thibitisha ukweli wa maneno yaliyopigiwa mstari.   (alama 4)

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    Open chat