Posted on Leave a comment

Majibu

Bonyeza hapa ili upate maswali ya majibu haya

 1. MUKTADHA
  • Msemaji ni Kenga
  • anamwambia Sudi
  • wako katika karakana sokoni Chapakazi
  • Sudi amekataa mradi wa kuchonga Kinyago cha Ngao,Kenga anamweza kuwa akikubali mradi huo maisha yake yatabadilika kwani atapata tuzo nyingi pamoja na likizo ya mwezi mmoja lakini anakataa,

2. UMUHIMU WA KENGA

Tazama: namna ya kueleza umuhimu wa mhusika

Kuendeleza maudhui ya ufisadi

Baada ya Kenga kumsaidia Majoka kufunga soko na kungoa vibanda  Majoka anamhadi Kenga kipanda cha ardhi sokoni

kuendeleza maudhui ya usaliti

Anamwambia Majoka kuwa ikiwa amekataa kushindwa yeye amekubali na anajiunga na umati na kupokelewa.

 • Kuendeleza ploti

Hatua ya Ashua kwenda Ofisini na mwa Majoka na kutiwa nguvuni ilikuwa imepangwa na Kenga.

 • Kuendeleza maudhui ya mauaji

Kenga anatoa pendekezo la Chopi kuenda safari (kuuawa) kwani anajua mambo mengi na huenda akatoboa mipangao ya kumwangamiza Tunu.

 • Ni mfano wa washauri wanaounga mkono uongozi dhalimu

Kenga anamfahamisha Majoka kuwa watawawekea kina Tunu vidhibitimwendo na hatimaye kuwakomesha.

 • Kenga ametumiwa kuonyesha mbinu anazotumia Majoka kuongoza

Anamwambia Sudi kuwa atapata zawadi nyingi iwapo atakubali mradi wa kuchonga kinyago cha Ngao.

 • Kenga ni kielelezo cha washauri wachochezi

Majoka anapomwambia kuwa wataongeza mishahara kisha wapandishe kodi Kenga anamwambia kuwa mtu hawi mwana wa shujaa bila sababu. Pia, anamwambia Majoka aache kuwa na moyo  wa huruma.

 • Kenga anaendeleza maudhui ya taasubi ya kiume

Baada ya kukitazama kinyago anachochonga Sudi anasema Sagamayo haijawai kuwa na shujaa wa kike

 • Ametumiwa kukuza maudhui ya mapuuza

Anamwambia Majoka asiyapuuze maandamano yanayoendelea. Majoka anasema kuwa waandamanaji watachoka hatimaye anaondolewa uongozini.

 • Mwandishi amemtumia kuonyesha namna viongozi wananyanyasa watawaliwa

Kenga anamwambia Majoka atangaze kuwa maandamano ni haramu na awaamuru maafisa wa polisi kutumia nguvu zaidi.

3. MBINU ANAZOTUMIA MAJOKA KUONGOZA

 • Vitisho – Siti anasema kuwa wametumiwa vijikaratasi vinavyosema wahame Sagamoyo.Hii ni baada ya jirani yao Sudi kuingilia siasa za kumpinga Majoka.
 • Mauaji– Jabali aliwauawa kwa sababu alikuwa mpinzani wa Majoka.
 • Vyombo vya dola– Polisi waliwaua vijana waliokuwa wakiandamana.Pia, wanatumia vitoza machozi kuwatawanya waandamanaji.
 • Propaganda – Kupitia redio, Majoka anawaambia Wanasagamoyo wasiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni kuwarejesha kwenye utumwa wa kimawazo.
 • Tenga tawala– hataki kuzungumza na Tunu na Sudi wote wakiwa pamoja.Tunu anamwambia aseme nao wote anapotambua kuwa anataka kuwagawa.
 • Kukiuka sheria– Anampa mama pima kibali cha kuuza pombe haramu kwa Ngurumo na asiya wanamuunga Majoka mkono.
 • Kufuta kazi wasiomuunga mkono – Majoka anamfuta kazi kingi kwa anapokataa kuwapiga watu risasi sokoni Chapakazi.
 • Ulaghai-Majoka anasema ataongeza mishahara ya waalimu na wauguzi kwa aslimia kidogo kisha apandishe kodi kwani hesabu nzuri ni kutia na kutoa.
 • Kuwafunga watu jela– Ashua anafungwa kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali. Hii ilikuwa fursa ya kulipiza kisasi kwa Sudi.
Content Protection by DMCA.com
Share this;
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments