Posted on Leave a comment

Maana ya mzizi wa neno

Dhana ya mzizi wa neno

mfano wa mzizi

Tunaposikia neno mzizi jambo la kwanza ambalo hutujia akilini ni sehemu fulani ya mti.Mti  husimama na kukua kwa sababu umeshikiliwa ardhini na mizizi.Hivyo basi,neno huitaji mzizi.

Sehemu hii ni muhimu sana katika neno kwani hubeba maana ya kimsingi ya neno fulani.Kwa mfano kutokana na mzizi –tu tunaweza kupata maneno kama; mtu,watu,kitu,vitu. Kwa hivyo, mzizi hutumiwa tunapounda maneno katika lugha.Sehemu hii pia haibadiliki hata neno likiongezwa viambishi.

Kwa mfano:

  • Wanaochekwa,tuliowacheka (mzizi ni chek)
  • Vilivyosomwa,someana,somesha,somwa

Kutokana na mifano hii tunaweza kusema mzizi ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi au sehemu ambayo hubakia baada ya kuondoa viambishi awali na tamati.

Kutambua mzizi katika neno

Jambo la kwanza ni kuondoa viambishi.

Kwa mfano: waliangukia

Wa-li-anguk-i-a ,mzizi ni anguk

Aina za mzizi

Katika lugha ya Kiswahili kuna mzizi huru na mzizi funge.Mzizi huru huwa neno kamili bila kuongezwa viambishi.Kwa mfano,leo,kamusi,sahau,dharau.. Mzizi funge huongezwa viambishi ili kuwa na maana kamili,kwa mfano anguk,som,on,pig,andik,f,l,ch, …

Maswali

Onyesha mzizi katika maneno yafuatayo

  1. nywishiana
  2. Alinijia
  3. Pakuliwa
  4. Oneana
  5. Safirishiwa
  6. Valiana
  7. pokezwa
Content Protection by DMCA.com
Share this;
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments