Posted on Leave a comment

Aina za Virai

kirai

Maana ya kira

  1. Neno au fungu la maneno ambalo halina maana kamili.
  2. Sehemu ya sentensi ambayo haina muundo wa kiima kiarifu

Sifa za kirai

  • Huweza kuwa neno moja au fungu la maneno
  • Kirai huwa na maana lakini maana hiyo si kamili
  • Kirai hakina muundo wa kiima kiarifu
  • Kirai huanishwa kulingana na neno lake kuu

Aina za virai

Tazama sentensi ifuatayo :

Msichana mrembo sana ameketi nyuma ya nyumba.

Sentensi hii ina sehemu nyingi ambazo zimeunganishwa pamoja kukamilisha ujumbe.

Msichana mrembo sana- kirai nomino

mrembo sana- kirai kivumishi

sana- kirai kielezi

Ameketi nyuma ya nyumba- kirai kitenzi

Nyuma ya nyumba- kirai kihusishi

Kirai neno/kifungu cha maneno kimepewa jina kulingana na neno lake kuu

Neno kuu linaweza kuwa ,nomino,kitenzi,kivumishi,kielezi au kihusishi.

Kuna aina tano za virai

Kirai nomino

Neno kuu ni nomino

Miundo ya kirai nomino

W : Huyu anasoma.

N :  Nchi imeimarika

W+V : Hicho chako kinapendeza.

N+V : Nchi yetu inavutia

N+U+N : Paka na mbwa hufugwa nyumbani.

N+V+V : Shamba lenu kubwa litauzwa.

N+S : Chombo kilichotumiwa kupikia.

Kirai kitenzi

Neno kuu ni kitenzi

Miundo

T : Bakari anaogolea.

T+E : Bakari anaogelea baharini.

t+N : Tunu ni mvumilivu.

T+KH : Alilia kwa furaha

T+N+E : Fanani alisimulia hadithi vizuri.

T+N+N : Waziri wa elimu aliwapa watoto vitabu.

T+N+S : Shangazi alinunua simu inayopendeza

Kirai kielezi

Neno kuu ni kielezi

Miundo

E : Amechoka sana.

E+E : Amekimbia haraka sana.

Kirai kivumishi

Neno kuu ni kivumishi

Miundo

V : Gari langu linavutia.

V+V : Shamba hilo lenu litauzwa.

V+N : Ashua ni mtu mwenye utu.

Kirai kihusishi

            H+N : Alitibiwa na daktari.

                       Kimeanguka chini ya meza.

Tazama matumizi mengine ya kirai kihusishi

Content Protection by DMCA.com
Share this;
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments