Sarufi

Ngeli za Kiswahili

Ngeli ni mpangilio wa nomino katika makundi. Mpangilio huu ni muhimu sana katika lugha ya Kiswahili kwani husaidia katika upatanisho wa nomino na vitenzi na maneno mengine. Mbinu hii huitwa upatanisho wa kisarufi.

Ngeli za Kiswahili
A-WA
LI-YA
U-ZI
U-I
KI-VI
U-U
I-ZI
KU
YA-YA
I-I
U-YA
PA-KU-MU

A-WA

Ngeli hii hujumuisha majina ya binadamu na viumbe vilivyo hai. Huwa na kiambishi a katika umoja na wa katika wingi.

Kiambishi cha umoja-a

Kiambishi cha wingi-wa

Mfano

Mtoto anacheza.

Watoto wana cheza.

Ndege anaimba .

Ndege wanaimba.

Miundo ya nomino

KI-VI

Kipepeo anapendeza.

Vipepeo wanapendeza.

CH-VY

Chura aliruka.

Vyura waliruka.

M-WA

Mtu ameonekana.

Watu wameonekana.

M-MI

Mtume anahubiri.

Mitume wanahubiri.

Ngeli ya KU

Hii ni ngeli ya kitenzi jina. Vitenzi vinapoongezwa kiambishi ku na kutumiwa kama nomino katika sentensi ,hubadilika na kuwa vitenzi jina. Nomino hii huwa na kiambishi ku katika upatanisho wa kisarufi.

Mfano

Cheka-kucheka

Kucheka kwake kunavutia.

Cheza-kucheza

Kucheza huko hakufai barabarani.

Tanbihi: Lazima kitenzi kitumike kama nomino ili kipiwe sifa hii.

Tazama: Ameanza kucheza. Neno “kucheza” ni kitenzi wala si kitenzi jina.

Ngeli ya I-ZI

Hii ni ngeli ya nomino ambazo huwa katika hali ya umoja.

Kiambishi cha umoja-i

Kiambishi cha wingi-zi

Mfano

Ngozi hiyo inavutia.

Ngozi hizo zinavutia.

Ngeli hiyo inaeleweka.

Ngeli hizo zinaeleweka.

Ngeli ya LI-YA

Kiambishi cha umoja-li

Kiambishi cha wingi-ya

Mfano

Gari limenunuliwa.

Magari yamenunuliwa.

Muindo ya nomino

G-M

Gari-magari

JI-MA

Jani-majani

Jicho-macho

Y-M

Yai –mayai

JI-ME

Jino-meno

Ngeli ya PA-KU-MU

Hii ni ngeli inayoashiria mahali. Kila kiambishi katika ngeli hii huwa na matumizi ya kipekee.

Pa- mahali panapodhihirika

Mahali hapa panavutia.

Mu- mahali ndani

Kanasani homo mna watu wengi.

Ku- mahali kusikodhihirika

Mahali huko kumejaa maji.

Ngeli ya KI-VI

Kiambishi cha umoja-ki

Kiambishi cha wingi-vi

Mfano

Kiti kimenunuliwa.

Viti vimenunuliwa.

Kioo kimevunjika.

Vioo vimevunjika.

Ngeli ya U-ZI

Kiambishi cha umoja- u

Kiambishi cha wingi-zi

Mfano

Uta umekatika.

Nyuta zimekatika.

Miundo ya nomino

U-NYU

Uta-nyuta

Uzi-nyuzi

W-NY

wembe- nyembe

Ngeli ya YA-YA

Nomino katika ngeli hii hupatikana katika hali ya wingi.

Kiambishi cha umoja-ya

Kiambishi cha wingi-ya

Mfano

Maji yamemwagika.

Maji yamemwagika.

Mifano ya nomino: mafuta,mate,manukato,maziwa

Ngeli ya U-I

Kiambishi cha umoja-u

Kiambishi cha wingi- i

Mfano

Mkono unaniuma.

Mikono inaniuma.

Mti umekatwa.

Miti imekatwa.

Mlima unavutia.

Milima inavutia.

Ngeli ya I-I

Nomino nyingi katika ngeli hii ni zile zisizohesabika. Nyingine huwa ni nomino dhahania.

Kiambishi cha umoja-i

Kiambishi cha wingi-i

Mfano

Amani imepatikana.

Amani imepatikana.

Sukari imeloa maji.

Sukari imeloa maji.

Ngeli ya U-U

Hii ni ngeli ambayo hujumuisha nomino dhahania.

Kiambishi cha umoja-u

Kiambishi cha wingi-u

Mfano

Upendo utanifaa.

Upendo utawafaa.

Mifano zaidi ya nomino: uzuri,wema,uovu,ukakamavu

Ngeli ya U-YA

Kiambishi cha umoja-u

Kiambishi cha wingi-ya

Mfano

Ugonjwa umetibiwa.

Magonjwa yametibiwa.

Mifano Zaidi ya nomino: uovu,ubaya,unyoya

Tanbihi: Nomino huwa na kiambishi u katika umoja na ma katika wingi

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Vivumishi ya pekee

Vivumishi vya pekee huwa sita. Kila kivumishi katika kundi hili huwa na matumizi ya kipekee

Aina ya vivumishi vya pekee

1. enye
2. enyewe
3. ote
4. o-ote
5.ingine
6. ingineo

enye
Maana: umilikaji

1. Nchi yenye madini mengi.
2. Viongozi wenye ubinafsi.
3. Mtoto mwenye uvivu
Ni makosa kutumia enye pamoja na kitenzi :
Mtu mwenye alikujaEnyewe
Maana: kusisitiza

1. Kiongozi mwenyewe amefika.
2. Askari wenyewe wamefika.
3. Kanisa lenyewe litaungwa mkono.

Ote
Maana: bila kubakisha

1. Watoto wote watatibiwa
2. Barabara yote imeharibika
3. Shamba lote litalimwa.

O-ote
Maana: bila kuchagua

1. Watoto wowote watatibiwa
2. Barabara yoyote itatengenezwa.
3. Shamba lolote litalimwa.

Ingine
Maana: baadhi ya/Zaidi ya/sehemu ya

Maana ya kivumishi hiki hutegemea muktadha.

1. Watu wengine wamezoea kutupa taka hapa: baadhi ya/sehemu ya
2. Watu wengine watafika kesho: zaidi ya

Ingineo
Maana: kuongezea/zaidi

1. Kiti kinginecho kimeletewa wageni.
2. Mzungumzaji mwingineo amefika.
3. Mada nyinginezo zitajadiliwa.


Content Protection by DMCA.com
Share this;
kirai

Aina za Virai

Maana ya kira

 1. Neno au fungu la maneno ambalo halina maana kamili.
 2. Sehemu ya sentensi ambayo haina muundo wa kiima kiarifu

Sifa za kirai

 • Huweza kuwa neno moja au fungu la maneno
 • Kirai huwa na maana lakini maana hiyo si kamili
 • Kirai hakina muundo wa kiima kiarifu
 • Kirai huanishwa kulingana na neno lake kuu

Aina za virai

Tazama sentensi ifuatayo :

Msichana mrembo sana ameketi nyuma ya nyumba.

Sentensi hii ina sehemu nyingi ambazo zimeunganishwa pamoja kukamilisha ujumbe.

Msichana mrembo sana- kirai nomino

mrembo sana- kirai kivumishi

sana- kirai kielezi

Ameketi nyuma ya nyumba- kirai kitenzi

Nyuma ya nyumba- kirai kihusishi

Kirai neno/kifungu cha maneno kimepewa jina kulingana na neno lake kuu

Neno kuu linaweza kuwa ,nomino,kitenzi,kivumishi,kielezi au kihusishi.

Kuna aina tano za virai

Kirai nomino

Neno kuu ni nomino

Miundo ya kirai nomino

W : Huyu anasoma.

N :  Nchi imeimarika

W+V : Hicho chako kinapendeza.

N+V : Nchi yetu inavutia

N+U+N : Paka na mbwa hufugwa nyumbani.

N+V+V : Shamba lenu kubwa litauzwa.

N+S : Chombo kilichotumiwa kupikia.

Kirai kitenzi

Neno kuu ni kitenzi

Miundo

T : Bakari anaogolea.

T+E : Bakari anaogelea baharini.

t+N : Tunu ni mvumilivu.

T+KH : Alilia kwa furaha

T+N+E : Fanani alisimulia hadithi vizuri.

T+N+N : Waziri wa elimu aliwapa watoto vitabu.

T+N+S : Shangazi alinunua simu inayopendeza

Kirai kielezi

Neno kuu ni kielezi

Miundo

E : Amechoka sana.

E+E : Amekimbia haraka sana.

Kirai kivumishi

Neno kuu ni kivumishi

Miundo

V : Gari langu linavutia.

V+V : Shamba hilo lenu litauzwa.

V+N : Ashua ni mtu mwenye utu.

Kirai kihusishi

            H+N : Alitibiwa na daktari.

                       Kimeanguka chini ya meza.

Tazama matumizi mengine ya kirai kihusishi

Content Protection by DMCA.com
Share this;
a unganifu

Matumizi ya a-unganifu

UAMILIFU WA A-UNGANIFU

A-unganifu huwa na matumizi mbalimbali katika lugha ya Kiswahili.

Sehemu hii katika sentensi huunda kirai kihusishi kwani neno kuu huwa ni kihusishi

Mfano

 1. Nyumba ya mbao
 2. Kiti cha enzi.
 3. Gari la abiria.

Sehemu zilizopigiwa mstari ni kirai kihusishi

Aghalabu, kihusishi <a> hufuatwa na nomino.

Matumizi ya a- unganifu

Kuonyesha aina ya kitu/jambo fulani

 1. Chumba cha malazi
 2. Dawa za malaria.
 3. Maji ya mto.
 1. Uwanja wa ndege.
 2. Mashairi ya arudhi

Kuonyesha umilikaji

 1. Kitabu cha mwanafunzi.
 2. Mali ya umma.
 3. Gari la rais.

Kuonyesha nafasi katika orodha

 1. Waziri wa kwanza kufiki bungeni ni yupi ?
 2. Kipchoge amemaliza akiwa wa nne.
 3. Mtahiniwa wa tatu amefika.

Swali

Tunga sentensi yenye kirai kihusishi kinachoonyesha nafasi katika orodha.(alama 2)

Content Protection by DMCA.com
Share this;
alama ya kishazi tegemezi

Uchanganuzi wa sentensi changmano: Matawi

Uchanganuzi wa sentensi changamano kwa kielelezo cha matawi

Rejelea makala yafuatayo :

Kielelezo cha kistari

Kielelezo cha jedwali

Hatua za uchanganuzi

 1. Kutambua kundi nomino na kundi tenzi
 2. Ni muhimu kujua miundo mbalimbali ya KN na KT
 3. Kutambua kishazi tegemezi
 4. Kutambua iwapo kishazi tegemezi kinajitokeza upande wa KN au KT

Mfano 1

Tarakilishi iliyonunuliwa inapendeza sana.

Uchanganuzi

Tarakilishi iliyonunuliwa  KN

inapendeza sana. KT

               

uchanganuzi wa sentensi changamano

Mfano 2

Wauguzi waliogoma wiki mbili watasimamishwa kazi

Uchanganuzi

Wauguzi waliogoma wiki mbili   KN

watasimamishwa kazi KT

uchanganuzi wa sentensi changamano

Mfano 3

Mjomba alishtuka alipopigiwa simu.

Uchanganuzi

Mjomba KN

alishtuka alipopigiwa simu. KT

uchanganuzi wa sentensi changamano

Mfano 4

Waliotuzwa walijitahidi sana

Uchanganuzi

Waliotuzwa          KN 

 walijitahidi sana KT

uchanganuzi wa sentensi changamano

Mfano 5

Wakenya wote wameifurahia sheria iliyopitishwa jana

Uchanganuzi

Wakenya wote       KN

wameifurahia sheria iliyopitishwa jana KT

uchanganuzi wa sentensi changamano

Maswali

Pata maswali na mifano yote ya uchanganuzi wa sentensi

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Uchanganuzi wa sentensi ambatano

Uchanganuzi wa Sentensi Ambatano: Kielelezo cha Kistari

UTANGULIZI

 1. Kistari/mstari ni mbinu ya kimsingi ya kuchanganua sentensi.
 2. Mbinu hii ni rahisi kuelewa
 3. Sentensi ambatano huwa na vishazi huru viwili
 4. Vishazi hivi huunganishwa kwa kutumia viunganishi

UCHANGANUZI

Alama zinazotumika

 • S-sentensi kuu
 • S1-sentensi ya kwanza(kishazi huru)
 • S2-sentensi ya pili (kishazi huru)
 • U-kiunganishi

MIFANO:


Swali

Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari (alama 2)

Ndugu yangu atakupigia kwa hivyo usichelewe kufika.

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Aina za shamirisho

SHAMIRISHO

Shamirisho ni nomino ambayo huashiria kitendwa/mtendwa au kitendewa/mtendewa katika sentensi.

Nomino hii huweza kuambatana na kivumishi/vivimushi.


Aina za shamirisho

Kuna aina tatu za shamirisho

 1. Shamirisho kipozi/yambwa tendwa
 2. Shamirisho kitondo/yambwa tendewa/yambiwa
 3. Shamirisho ala

Shamirisho kipozi (direct object)

Ni nomino ambayo hupokea athari ya kitenzi moja kwa moja

Mifano;

 1. Mama anapika chakula.
 2. Mama anapika chakula kitamu
 3. Mama anapika chakula kitamu sana

Chakula/chakula kitamu/chakula kitamu sana ni shamirisho kipozi kwa sababu chakula kinatendwa/kinapokea kitendo moja kwa moja.

Mifano zaidi

 1. Nyumba kubwa iliyojengwa jana imebomoka.
 2. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu.
 3. Mwanaheri alinunua simu yenye rangi nyingi.

Shamirisho kitondo (indirect object)

Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Sentensi nyingi huwa na vitenzi katika kauli ya kutendea/kutendewa.

Mfano

 1. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu.( Nani alitendewa ? mtoto)
 2. Shangazi alimnunulia babu yangu koti. (Nani alitendewa? Babu yangu)

Shamirisho ala/kitumizi

Hii ni nomino ya kifaa ambacho hutumiwa kutendea kitendo fulani

Mara nyingi  hujitokeza katika vielezi vya namna ala

Kihusishi “kwa” si sehemu ya shamirisho ala

Mfano

 1. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu .(Alitumia nini kukata mkate? Kisu)
 2. Nyunba hiyo ilijengwa kwa mawe. (nyumba ilijengwa kwa kutumia nin? Mawe)
 3. Abiria watasafiri kwa basi kubwa. ( abiria watatumia nini? Basi kubwa)

Maswali

Bainisha shamirisho katika sentensi zifuatazo

 1. Alisema atamjengea mshindi nyumba ya mbao.
 2. Mgonjwa alitibiwa na daktari kwa dawa ghali.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
alama ya kishazi tegemezi

Uchanganuzi wa Sentensi Changamano : Kielelezo cha Jedwali

Utangulizi

Sentensi changamano huwa na kishazi huru na kishazi tegemezi. Rejelea makala kuhusu aina za sentensi kimuundo pamoja na aina za uchanganuzi wa sentensi. Makala ya leo yatashughulikia kielelezo cha jedwali.

Hatua za uchanganuzi

 1. Tambua kundi nomino na kundi tenzi
 2. Tambua kishazi tegemezi.Je,kishazi tegemezi kinajitokeza upande wa kundi nomino au kundi tenzi ?
 3. Tambua aina mbalimbali za maneno

Mfano 1

Runinga iliyonunuliwa ni ya jirani.

Kishazi tegemezi : iliyonunuliwa

                                                  S
                 KN   KT
          N t H N
Runinga iliyonunuliwa ni ya jirani

Mfano 2

Kijana huyo anayekupigia simu alifika jana.

Kishazi tegemezi: anayekupigia simu

                                                  S
                 KN   KT
         N V   T E
Kijana huyo anayekupigia simu alifika jana

Mfano 3

Dola alilicheka alipoanguka sakafuni

Kishazi tegemezi: alipoanguka sakafuni

                                                             S
KN                          KT
N T
Dola alicheka alipoanguka sakafuni

Mfano 4

Askari ambaye alimkamata ni mwadilifu

Kishazi tegemezi: ambaye alimkamata

                                                         S
               KN                          KT
N t V
Askari ambaye alimkamata ni mwadilifu

Maswali

Changanua sentensi zifuatazo kwa kielelezo cha jedwali

 1. Hiyo siku aliyokutembelea alikaribishwa vizuri.
 2. Mfanyikazi alifurahi aliponunuliwa zawadi.
 3. Pili ambaye alipita mtihani ni mwanafunzi mwenye bidii.
Content Protection by DMCA.com
Share this;
irabu

Uainishaji wa irabu

Mwandishi: Zablon Rogito

SAUTI

Maana: Sauti ni mlio unaotokana na mgusano wa ala za kutamkia wakati wa kuzungumza

Aina za sauti

Sauti za lugha ya kiswahili zimegawika katika makundi mawili:

 • Irabu
 • Konsonanti

Irabu

Irabu ni sauti ambazo inapotamkwa hewa kutoka mapafuni haizuiliwi Kwokwote, yaani hewa upita kwa ulaini.

Sauti za irabu ni tano nazo ni:

/a/,/e/,/i/,/o/,/u/

Vigezo vya kuainisha irabu

Irabu uainishwa kwa kuzingatia Vigezo vifutavyo

1. Hali ya midomo

 • Mviringo: u,a
 • Kutandazika: a,i,e

2. Mkao wa ulimi katika kinywa

 • Juu: u,i
 • Chini: a
 • Kati: o,e

3. Sehemu ya ulimi ya kutamkia

 • Mbele: e,i
 • Kati: a
 • Nyuma: u,o

 

Sauti na sifa zake bainifu

/a/_hutamkiwa chini kati

_inapotamkwa midomo utandazika

/e/_hutamkiwa mbele kati

_midomo utandazika

/i/_hutamkiwa mbele juu

_midomo utandazika

/o/_hutamkiwa nyuma kati

_midomo huwa mviringo

/u/_ni sauti ya nyuma juu

_inapotamkwa midomo huviringika

 

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Sentensi Ambatano

MAANA : Sentensi ambatano ni sentensi ambayo ina vishazi huru viwili au zaidi.

Kishazi huru huwa na maana kamili. Kikiondolewa katika sentensi kuu huwa kina maana iliyokamilika.

Mara nyingi sentensi ambatano  huwa na kiunganishi. Kiunganishi hiki hutumiwa kuziunganisha vishazi hivi. Hivyo basi, sentensi ambatano huwa na sentensi mbili au zaidi ambazo zimekamilika kimaana na kuunganishwa pamoja.

Mifano 1

 Mhuburi anahubiri na watoto wanalia kanisani

Sentensi hii ina vishazi huru viwili

 • Mhubiri anahubiri.
 • Watoto wanalia kanisani

Mifano zaidi

 1. Anapiga simu lakini mteja hapatikani.
 2. Anacheza huku akicheka.
 3. Ametumwa bungeni na rais ili kupitisha ujumbe wa dharura.
 4. Daktari huyu hutibu wagonjwa vizuri lakini yule ana mzaha kazini.

Kama ilivyo katika sentensi zingine, sentensi ambatano pia inaweza kuchanganuliwa kwa kutumia njia zifuatazo.

 1. Kistari
 2. Mishale
 3. Jedwali
 4. Matawi

Tuangalie uchanganuzi wa sentensi ambatano kwa njia ya kistari

Mhuburi anahubiri na watoto wanalia kanisani

S———-S1+U+S2

S1——–KN+KT

KN——-N

N——–mhubiri

KT——- T

T——— anahubiri

U——– na

S2———KN+KT

KN——–N

N———- watoto

KT———T+E

T——–wanalia

E——– kanisani

Anacheza huku akicheka.

S———–S1+U+S2

S1———-KN+KT

KN———ø

KT———-T

T———- anacheza

U———- huku

S2———–KN+KT

KN——— ø

KT———-T

T———— akicheka

Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat