KCSE Insha 2008

KISWAHILI

Karatasi ya 1 INSHA Okt/Nov, 2008

Karatasi ya 1

INSHA

Maagizo

 • Andika Insha mbili insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Insha ya lazima.
 1. Andika tahariri kwa gazeti la Raia ukieleza hatua zinazochukuliwa nchini ilikumwendeleza kielimu mtoto msichana.
 2. “Ufisadi ndicho kikwazo kikuu katika maendeleo ya uchumi wa taifa lolote.” Thibitisha.
 3. Matikiti na matango ndiyo maponya njaa.
 4. Andika insha itakayomalizikia kwa ;  “Aha! Kumbe mwungana akivuliwa nguo huchutama. Sitaisahau siku hiyo kwani sijawahi kufedheheka maishani kama nilivyoaibika siku hiyo

MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA

Swali La Kwanza

Tahariri Kwa Gazeti La Raia

a)            Sura

 • Iwe na kichwa.
 • Iwe na tarehe.
 • Iwe na utangulizi.
 • Iwe na mwili/maelezo kiaya.
 • Yaweza kuwa na maoni au msimamo wa mhariri au msimamo wa gazeti.
 • Iwe na hitimisho k.m. jina la mhariri na wadhifa wake.

b)            Maudhui:              Kuendeleza Msichana Kielimu

 • Kupiga vita ndoa za mapema.
 • Kupiga marufuku ajira ya watoto.
 • Wasichana wapewe nafasi ya kuendelea na masomo ya baada kujifungua.
 • Alama za kujuinga na shule na vyuo vikuu kupunguzwe kwa wasichana.
 • Elimu bila malipo kwa watoto wa shule za msingi na za upili.
 • Kutoa msaada wa karo kwa familia maskini.
 • Kujenga shule zaidi za wasichana.
 • Mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga shule na vyuo.
 • Kuhamasisha wazazi kuhusu umuhimu wa elimu ya mtoto msichana.
 • Adhabu kali kwa wabakaji.                                                                                                      (Alama 20)

Swali La Pili:     

a)            Ufisadi Kama Kikwazo

 • Hii ni insha ya hoja.
 • Hoja ziunge mkono kauli hii.
 • Mtahiniwa akubaliane na kauli hii.
 • Mtahiniwa ahusishe ufisadi unavyodumaza uchumi wa nchi.

b)            Hoja

 • Watu kupewa kazi wasizoweza.
 • Wanaostahili kazi hawapati.
 • Biashara haramu huwapunja raia.
 • Wawekezaji huvunjwa moyo.
 • Miradi ya maendeleo kukwama/kutomalizwa.
 • Baadhi ya maeneo ya nchi kupuuzwa kimaendelepo.
 • Nchi kukosa misaada.
 • Taifa hutumia pesa nyingi kurekebisha ufisadi.
 • Sifa za nchi kuharibika.
 • uhalifu kuenea/kukosa usalama.

Swali La Tatu    

a)            Methali: “Matikiti Na Matango Ndiyo Maponya Njaa”

 • Hii ni methali.
 • Mtahiniwa atunge kisa/visa kuonyesha ukweli wa methali hii.
 • Kisa kionyeshe sehemu mbili za methali.
 1. Upuuzaji/kudunisha kitu, jambo au mtu.
 2. Kitu, mtu au jambo hilo lije liwe ni la manufaa baadaye wakati wa shida.

b)            Msamiati wa methali

 • Matikiti na matango = aina ya vyakula visivyothaminiwa sana.
 • Maponya = yanayookoa/yanayofaa
 • Njaa = shida

c)             Maana ya methali

Vitu tunavyodunisha/tunavyopuuza huweza kuwa na msaada mkubwa wakati wa shida.  Kitu tulichonacho mkononi mwetu ndicho kinaweza kututoa taabani wakati wa shida, hivyo basi tusikidharau.                                                                                                                                                                    

Swali La Nne      

a)            Insha Ya Mdokezo

 • Hii ni Insha ya mdokezo na mdokezo huu ni wa kumalizia.
 • Mtahiniwa atunge kisa kinachomalizikia kwa dondoo hili.
 • Mtahiniwa ajihusishe katika kisa hiki.
 • Mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza
 • Kisa kiwe na tendo/jambo baya kisiri
 • Jambo hili linawekwa wazi
 • Mhusika anakosa uso yaani anaaibika sana.

b)            Methali:                “Muungwana akivuliwa nguo huchutama”.

Maana: Uovu wa mtu anayedhaminiwa ni mwema unapofishuliwa yeye huaibika.

Content Protection by DMCA.com
Share this;