Fasihi Andishi

Maudhui_Chozi la Heri

a) Wakimbizi hupitia matatizo mengi kambini. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea riwaya Chozi la Heri. (Alama 20)

b) Fafanua mchango mashirika yasiyo ya kiserikali katika jamii kwa kurejelea riwaya Chozi la Heri. (Alama 10)

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Vigezo katika kueleza Umuhimu wa Mhusika

Swali la kujadili umuhimu wa mhusika fulani ni rahisi iwapo mwanafunzi anakumbuka mtiririko wa matukio vizuri. Ikumbukwe kuwa swali hili hutolewa mifano pia. Mtahiniwa anaweza kuzingatia vigezo vifuatavyo;

 1. Je, mhusika huyu ametumiwa kupitisha maudhui gani?
 2. Je, mhusika huyu ametumiwa kuonyesha sifa za wahusika wengine?
 3. Je, ametumika katika kuendeleza ploti?
 4. Je, anawakilisha watu wa aina gani katika jamii? Kwa mfano, Majoka anawakilisha viongozi ambao ni wakatili katika jamii
 5. Je, ametumiwa kama kielelezo cha kina nani katika jamii? Kwa mfano, watetezi wa haki.
 6. Je, anaibua mambo gani katika jamii? Kwa mfano, Katika hadithi “Mkubwa” Mkumbukwa anaonyesha changamoto wanazoipitia mahabusu……
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Swali la Dondoo: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

“Haikuwa stahiki yake kubebeshwa mzigo ule. Ungelimsababishia dhiki nyingi…”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b)Tambua tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)

c)Eleza umuhimu wa anayerejelewa katika kufanikisha maudhui ya hadithi hii. (alama 6)

d)Mhusika anayerejelewa katika dondoo hili anahofia mambo mengi,fafanua kwa kutoa mifano mwafaka. (alama 8)

Content Protection by DMCA.com
Share this;
chozi la heri cover page

Chozi la Heri: Swali la Dondoo (al 20)

Chozi la Heri: Assumpta Matei

Soma kauli ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuta

“ Sasa unarejea kwenu kupata tumekuporomosha kwa viganja vyetu wenyewe.”

a)   Eleza mukutadha wa dondoo hili. (alama 4)

b)   Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika kauli hii. (alama 2)

c)   Bainisha matumizi mengine kumi ya tamathali hii ya usemi katika riwaya. (alama 10)

d)   Huku ukitoa mifano katika riwaya thibitisha ukweli wa maneno yaliyopigiwa mstari.   (alama 4)

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Kigogo: Uchanganuzi wa tendo la kwanza

KIGOGO: Pauline Kea

Onyesho la Kwanza

Tendo la 1&2

Mandhari: kwenye karakana,soko la Chapakazi

Wakati : saa mbili asubuhi

Wahusika : Boza,Sudi,Kombe,Ashua,Mzee Kenga,Chopi,Tunu

Maswali ya Uchanganuzi

 • Kwa nini Boza anatematema mate ?
 • Ashua anafanya kazi gani?
 • Taja shida wanazopitia sokoni.
 • Taja mambo yanayoonyesha kuwa Boza,Sudi,Ashua na Kombe ni maskini.
 • Boza ana msimamo gani kuhusu utawala wa sagamoyo.
 • Kombe anamaanisha nini anaposema “kuwa moshi utazaa moto”.
 • Kwa nini mke wa Boza alipewa kandarasi ya kuoka keki?
 • Thibitisha kuwa mzee kenga ni “mwenye nchi”.
 • Linganisha sifa za shujaa wa kweli wa Sagamoyo kwa mtazamo wa Kenga na Sudi.
 • Thibitisha kwa kutoa mifano namna kushurekea uhuru wa miaki sitini ni kinaya.
 • Kwa maoni yako,keki ya taifa inaashiria nini?
 • Eleza maana ya methali “ukitaka kula asali kaa na nyuki” kulingana na tendo hili.
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Namna ya kutambua sifa za wahusika katika fasihi

 1. Maelezo ya mwandishi

Waandishi mara nyingi hutaja sifa za wahusika moja kwa moja au kwa njia ya maelezo.

Shogake Dada ana Ndevu-Alifa Chokocho

Safia

Ni mwenye bidii- hachoki kumsaidia mamake kazizi yoyote mle nyumbani mwao,hupika,huosha vyombo,hufua ,hupiga pasi na kutandika kila siku.

Ni mcha mungu- anafuata kanuni zote alizoamrisha Mungu kupitia dini yao.

Tumbo Lisiloshiba- Said A.Mohamed

Mzee Mago

Ni mtetezi  wa haki-yeye hupiga mbio huku na kule ,kujaribu hili na lile,kuzuia haki isiangamizwe.

Ni mwenye ushawishi-anawaleta Wanamadongoporomoka pamoja kupigania haki ya kuishi Madongoporomoka.

Mapenzi ya Kifaurongo- Kenna Wasike

Penina

Ni mnafiki- anamwambia Dennis kwamba anampenda licha ya umaskini wake.Baadaye anamgeuka, “potelea mbali mkata wee!”

 1. Majina ya wahusika

Wahusika katika Fasihi hupewa majina ya kimajazi.Majina haya hutusaidia kutambua tabia na sifa zao.

Shogake Dada ana Ndevu- Alifa Chokocho

Kutoka na neno safi tunaelekea kutambua kuwa Safia ni mhusika  mwenye sifa nyingi chanya.NI msaidizi wa wazazi wake,ni mwenye bidii,ni hodari shuleni na ni mcha mungu.

Tamthilia ya Kigogo- Pauline Kea

Boza– boza ni mtu mpumbavu. Mhusika huyu anawaunga mkono Majoka na Kenga ingawaje hawajali maslahi yake. Wanafunga soko anakofanyia kazi, anaunga mkono sherehe za mwezi za kusherehekea uhuru  ilhali hawana cha kusherehekea, haki zao zinakiukwa na hawana chakula.

 1. Matendo ya wahusika

Tumbo Lisiloshiba- Said A.Mohamed

Jitu la miraba minne

Ni lenye ulafi- linakula chakula kingi na halishibi.

Ni lenye tamaa- linamwambia Mzee Mago kuwa limekuja kula ardhi yake.Lina hamu kubwa kupata ardhi ya Wanamadongoporomoka.

Mapenzi ya Kifaurongo- Kenna Wasike

Dennis

Ni mwenye bidii- ametoka katika familia maskini lakini anajitahidi hadi kufaulu masomoni.

Ni mwenye mapenzi ya kweli- anampenda Penina licha ya tofauti ya matabaka.Anampeleka Penina nyumbani kwao kwani wana mipango ya kuoana.

 1. Mazungumzo baina ya wahusika

Kutokana na namna mtu anavyozungumza unaweza kueleza sifa ningi kumhusu, mpyoro,mwenye kiburi na kdh.

Tumbo Lisiloshiba- Said A.Mohamed

Jitu la miraba minne

Ni lenye kiburi- linamwambia Mzee Mago, “mimi sitaki naam zako nyingi wala sitaki msaada wako dhaifu.

 1. Namna mhusika anavyosema kumhusu mhusika mwingine

Mhusika anaweza kutaja sifa ya mhusika mwingine moja kwa moja au kwa njia ya maelezo.

Mame Bakari- Mohammed Khelef Ghassany

Babake Sara

Ni mkaidi-  “Bwana yule mwenye masikio makaidi na mwenye tabia ya kutoamini maafa ya mtu mwengine?”

Ni mkali – “ angelipasuka kwa ukali tu”

Haya ni maneno ya mhusika Sara

 1. Namna wahusika walivyovalia

Mavazi ya wahusika pia ni muhimu katika kutambua sifa za wahusika na umuhimu wao katika fasihi.

Shogake Dada ana Ndevu- Alifa Chokocho

Kimwana

Ni mwongo- anaingia kwa kina Safia akiwa amevaa buibui ilhali yeye ni mwanamume.

SWALI

Je, unatambua nini kutokana na mavazi ya wahusika hawa katika tamthilia ya Kigogo na Pauline Kea?

 • Ashua (katika soko la chapakazi)
 • Husda (Majoka and Majoka modern Resort)
Content Protection by DMCA.com
Share this;

Maudhui ya tamaa katika Tumbo Lisiloshiba

Said A.Mohamed ni mwandishi mwenyee umaarufu mkubwa katika Fasihi ya Kiswahili. Vitabu vyake huwavutia wasomaji sana.

Hadithi fupi huwaiwaitaji wasomaji wawe makini sana ili waelewe kinachozungumziwa na maudhui. Wanufunzi hukosa mifano faafu na ya kutosha katika hadithi fupi.

Tumbo Lisiloshiba-Said A. Mohamed

Tamaa ni hamu kubwa ya kupata kitu. Mtu aliye na tamaa ni mtu ambaye hatosheki. Kutokana na maana hii tunaweza kusema kuwa mtu mwenye tumbo lisiloshiba ni mtu mwenye tamaa kwa sababu anakula na hatosheki.

Ikumbukwe kuwa   anwani Tumbo Lisiloshiba  imetumika kijazanda ikiwa na maana ya watu (wenye mali) ambao hawatosheki, wana hamu kubwa ya kupata mali zaidi.

Jitu la miraba minne lina tamaa ya chakula.Linapoingia katika mkahawa mshenzi kwa Mzee Mago linaitisha na kula chakula chote.

Kabla ya kuendeleza mjadala huu ningependa nirejelee maneno yafuatayo (tunawasaidia Wanamadongoporomoka kutegua kitendawili);

 • “Wala sitaki msaada wako dhaifu”

Kwa hivyo jitu hili linatumbua kuwa “msaada” wa Mzee Mago ni dhaifu, Mzee Mago anaishi Madongoporomoka “ wanakoishi watu wepesi wasio na mashiko”.

 • “ Nimekuja kukusaidia wewe. Nitakusaidia sana. Usiwe na wasiwasi”

Maneno haya ni kinaya. Jitu lenye tumbo lisiloshiba linamhakikishia Mzee Mago kuwa linakuja kula ardhi yake. Polisi wanatumiwa na watu wa aina hii kuwafukuza na kuwapiga wananchi wasio na hatia ili wahame katika ardhi yao.Wahame? Hapana, hawana pa kuhamia,jiji limejaa “ tukiondoshwa hapa tutakwenda wapi hapa jijini?”- maneno ya Kabwe.Watu walio nacho wanaongozwa na tamaa kwa hivyo hawawezi kuwasaidia maskini wanaoishi Madongoporomoka.

 • “Wakikubali wasikubali,itabidi leo chakula chote nikile mimi”

Wanamadongoporomoka wakubali wasikubali ardhi ya watu wasio na nguvu itanyakuliwa. Linakula chakula chote hata cha wale waliokuwa wamepanga kula hapo mkahawani.Tunatambua kuwa ardhi inayonyakuliwa, inanyakuliwa kwa lazima na watu wenye tamaa na wenyewe hawana pa kwenda “ hawajui wakimbilie wapi”

 • “Nina njaa kubwa ajabu”

Jitu hili lina tamaa, ni kweli kwa sababu lina mipango ya kunyakua ardhi ya watu wengi ambao hawana kwingine, hii si ni njaa kubwa ajabu?

 • “Nitalipa gharama zote. Nitalipa mara tatu tu …”

Tunatambua kuwa Jitu hili ni bwanyenye. Ni tamaa tu inaliongoza.Lina uwezo wa kulipa chakula chote ambacho kingewalisha watu wengi tena mara tatu. Lina mali nyingi lakini halitosheki.

 • “Kesho kama  sote tutaamka salama”

Maneno haya ni kinaya. Kila mtu aliamshwa na vishindo na vitisho vya mabuldoza na waliokuwa wamelala kutimuliwa na askari wa baraza.Jitu nalo lilifika kwa gari kubwa huku likitabasamu.

 • “ kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimama juu ya ardhi hii adhimu..”

Anawakejeli Wanamadongoporomka. Wengi hawakuweza kufungua milango yao  ya vibanda mshenzi ,vinabomolewa na askari wa baraza la mji. Je,ardhi hii ni ardhimu? Ardhi ambayo itahitaji kusafishwa, kukogeshwa na kusuuzwa?

 • “Nimekuja kula ardhi yako leo”

Ikumbukwe kuwa jitu likiondoka liliagiza kuwekewa chakula mara mbili. Kutokana na maneno haya tunatambua kuwa limefika kuhakikisha Wanamadongoporomoka wamefukuzwa ili liweze kumiliki ardhi yote.Hii ni tamaa.

Jitu hili lina tamaa ya kujiongezea mali. Jijini kumejazwa majumba na wakubwa mpaka hakuna nafasi hata ya mtu kuvuta pumzi.

Jitu hili kweli halishibi linaendelea kula tu, lina tamaa ya kuendelea kumiliki mali zaidi. Baada ya kulijaza jiji wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya Wanamadongoporomoka.

Wakubwa wana tamaa kubwa, wanataka kuchukua ardhi ya watu maskini kwa lazima. Ardhi ya Wanamadongoporomoka inachukuliwa kwa lazima,askari wa baraza wanabomoa vibanda,kupiga na kuwafukuza watu huku wamelindwa na jeshi la polisi lilokuwa limebeba bunduki.

Lakini fujo hizi hazikuwahamisha Wanamadongoporomoka

Kutokana na uzito wa maudhui ya tamaa mifano iliyotolewa hapa au itakayotelewa inaweza kutumika kuelezea ufaafu wa anwani.

Content Protection by DMCA.com
Share this;

Fasihi Andishi: Kigogo

Onyesho la Kwanza

Tendo la 1&2

Mandhari: kwenye karakana,soko la Chapakazi

Wakati : saa mbili asubuhi

Wahusika : Boza,Sudi,Kombe,Ashua,Kenga,Chopi

Maswali kwa wanafunzi

 1. Kwa nini Boza anatematema mate?
 2. Ashua anafanya kazi gani?
 3. Taja shida wanazopitia sokoni.
 4. Taja mambo yanayoonyesha kuwa Boza,Sudi,Ashua na Kombe ni maskini.
 5. Boza ana msimamo gani kuhusu utawala wa sagamoyo.
 6. Kombe anamaanisha nini anaposema “kuwa moshi utazaa moto”.
 7. Kwa nini mke wa Boza alipewa kandarasi ya kuoka keki?
 8. Thibitisha kuwa mzee kenga ni “mwenye nchi”.
 9. Linganisha sifa za shujaa wa kweli wa Sagamoyo kwa mtazamo wa Kenga na Sudi.
 10. Thibitisha kwa kutoa mifano namna kushurekea uhuru wa miaki sitini ni kinaya.
 11. Kwa maoni yako,keki ya taifa inaashiria nini?
 12. Eleza maana ya methali “ukitaka kula asali kaa na nyuki” kulingana na tendo hili.
Content Protection by DMCA.com
Share this;
0
  0
  Your Cart
  Your cart is emptyReturn to Shop
  Open chat