Posted on 4 Comments

Aina za shamirisho

SHAMIRISHO

Shamirisho ni nomino ambayo huashiria kitendwa/mtendwa au kitendewa/mtendewa katika sentensi.

Nomino hii huweza kuambatana na kivumishi/vivimushi.


Aina za shamirisho

Kuna aina tatu za shamirisho

 1. Shamirisho kipozi/yambwa tendwa
 2. Shamirisho kitondo/yambwa tendewa/yambiwa
 3. Shamirisho ala

Shamirisho kipozi (direct object)

Ni nomino ambayo hupokea athari ya kitenzi moja kwa moja

Mifano;

 1. Mama anapika chakula.
 2. Mama anapika chakula kitamu
 3. Mama anapika chakula kitamu sana

Chakula/chakula kitamu/chakula kitamu sana ni shamirisho kipozi kwa sababu chakula kinatendwa/kinapokea kitendo moja kwa moja.

Mifano zaidi

 1. Nyumba kubwa iliyojengwa jana imebomoka.
 2. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu.
 3. Mwanaheri alinunua simu yenye rangi nyingi.

Shamirisho kitondo (indirect object)

Ni nomino ambayo huathiriwa na kitendo kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Sentensi nyingi huwa na vitenzi katika kauli ya kutendea/kutendewa.

Mfano

 1. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu.( Nani alitendewa ? mtoto)
 2. Shangazi alimnunulia babu yangu koti. (Nani alitendewa? Babu yangu)

Shamirisho ala/kitumizi

Hii ni nomino ya kifaa ambacho hutumiwa kutendea kitendo fulani

Mara nyingi  hujitokeza katika vielezi vya namna ala

Kihusishi “kwa” si sehemu ya shamirisho ala

Mfano

 1. Anita alimkatia mtoto mkate kwa kisu .(Alitumia nini kukata mkate? Kisu)
 2. Nyunba hiyo ilijengwa kwa mawe. (nyumba ilijengwa kwa kutumia nin? Mawe)
 3. Abiria watasafiri kwa basi kubwa. ( abiria watatumia nini? Basi kubwa)

Maswali

Bainisha shamirisho katika sentensi zifuatazo

 1. Alisema atamjengea mshindi nyumba ya mbao.
 2. Mgonjwa alitibiwa na daktari kwa dawa ghali.

Content Protection by DMCA.com
Share this;
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Chee
Chee
1 month ago

The explanations were quite awesome …..??thanks so much be blessed
I hope this will help many students who didn’t understand the term shamirisho

student
student
1 month ago

we need pple like u